Twitter Facebook Feed

MTI WA MWEMBE NI TIBA KUANZIA MAJANI HADI MIZIZI

MTI WA MWEMBE NI TIBA KUANZIA MAJANI HADI MIZIZI

TUNDA la embe linafahamika kutokana na kuwa na walaji wengi, lakini pamoja na kuliwa, lina kazi nyingi katika mwili wa binadamu.
Mbali ya kuwa ni tunda na juisi yake kuwa kiburudisho, mti wake una kazi nyingi zaidi ya unavyojua.


Naanza na majani

Majani machanga yakichemshwa ni dawa ya pumu na pia huondoa matatizo ya kifua kikavu na kilichoiva.

Majani hayo pia hutumika kuoshea vidonda vya nje ya mwili ambapo hata kama mtu amepata ajali, huvikausha mara moja.
Unga wa majani hayo unaelezwa kusaidia katika kutunza meno ambapo mhusika atatakiwa kusukutulia na hivyo kuyafanya meno yake kuwa na nguvu wakati wote na kuepuka kuliwa na wadudu.

Kokwa

Wakati watu wengi wakiwa wanatupa kokwa kila wanapomaliza kula tunda hilo,  unga wa mbegu la mti huo ukinywewa mara 3 kwa siku ni dawa ya kuzuia kuharisha na kuhara damu.

Tunda

Watu wengi wakiwa wanapenda kula tunda hilo, ukweli ni kwamba hawajui kama wanajitibu minyoo na kuzuia uvujaji ovyo wa damu.

Hata hivyo,  kutokana na kuwa na madini ya vitamin C, husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, na hivyo mlaji sana wa tunda hili endapo atapata majeraha basi atapona haraka kuliko yule ambaye hali kabisa.

Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, tunda hili ni tiba sahihi, ambapo kambakamba zinazopatikana kwenye tunda hilo husaidia katika mfumo wa usagaji chakula, kazi inayofanywa katika utumbo mkubwa.
Hata hivyo, tiba katika tunda hupatikana wakati likiwa limeiva na wakati likiwa bichi ambapo ukipata vipande sita vibichi ndani ya wiki moja vinaweza kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji

Kwa wale wanaosumbuliwa na mapigo ya moyo kwenda kwa haraka,  mgonjwa atatakiwa kuchemsha embe bichi likiwa limechanganywa na chumvi, sukari na kisha kunywa ambapo kuanzia hapo ataona mwendo wa mapigo hayo ukianza kubadilika taratibu.

Magome

Magome ya mti huu yakichemshwa ni dawa ya homa, ugonjwa ambao unaweza kumsumbua mtu muda mrefu, lakini akipimwa anaambiwa hana malaria japokuwa anaona dalili zote.

Kitaalamu homa huwa haionekani kwenye vipimo na hivyo anachofanyiwa mgonjwa ni kupewa dawa za kutuliza maumivu.

Juisi ya embe

Juisi ya embe ikichanganywa na maziwa huwa ni kirejesho kizuri cha afya, na hapa nashauri kwamba ni vyema mnywaji akawa anatumia mara kwa mara.

Hivyo hiyo juisi  ukiwa na tabia ya kuinusa, inasaidia uzuiaji wa utokaji wa damu puani.

Dr Hamza
0654729438 WhatsApp coll sms
0655729439 WhatsApp coll sms
Tanga Pangani Tanzania

0 comments:

Post a Comment