FAIDA ZA MTI WA MWEMBE NA MAEMBE KATIKA MWILI WAKO
Dr Hamza
Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha ninayo vutia, una faida lukuki za kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti wa mwembe.
1. MAJANI YA MTI WA MWEMBE :
Majani machanga ya mti wa mwembe yakichemshwa huwa na faida zifuatazo ;
i. Hutibu pumu
ii. Hutibu kifua kikavu
iii. Hutumika katika kuoshea vidonda vitokanavyo na majeraha mbalimbali ( Majani ya maembe yamethibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kukausha majeraha ya vidonda )
iv. Unga wa majani ya mwembe hutumika katika kutunza meno ambapo mtu mwenye matatizo ya meno atatakiwa kusukutua kwa kutumia unga unaotokana na majani ya mwembe.
v. Vilevile Majani hutumika kutibia kabisa tatizo la kisukari type 2, Mgonjwa anatakiwa kuloweka majani ya kutosha kwenye maji nusu lita aache yalale huku halafu asubuhi afikiche vizuri hayo Majani kasha achue na anywe hayo maji. Anatakiwa kufanya zoezi hili kwa muda wa Mwezi Moja.
2.KOKWA LA EMBE
Unga unaotokana na kokwa la embe husaidia kuzuia kuharisha na kuhara damu.
3. TUNDA LA EMBE
i.Ulaji wa tunda la embe husaidia kutibu minyoo na kuzuia uvujaji wa damu ovyo.
ii. Tunda la embe lina vitamin C na hivyo ulaji wake husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, hivyo basi mlaji sana wa tunda la embe endapo atapata vidonda basi atapona kwa haraka sana kuliko mtu asiye tumia tunda hili mara kwa mara.
iii. Huwasaidia watu wenye matatizo ya kutokupata choo.
iv. Utumiaji wa maembe mabichi husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
v. Embe bichi likichanganywa na chumvi na sukari na kasha kuchemshwa ni tiba ya tatizo la mapigo ya moyo kwenda kwa haraka.
4.MAGOME YA MWEMBE
Magome ya mti wa mwembe yakichemshwa ni dawa nzuri ya homa.
5. MIZIZI YA MWEMBE
Mizizi yake ni dawa nzuri sana kwa meno haya meno yaliyotoboka, Unachotakiwa kufanya ni kuchukua mizizi ya kutosha kasha chemsha na usukutue utwa mara 3 kwa siku 7 kwa uwezo wa Mungu utakuwa umepona kabisa tatizo la Meno.
JUISI YA EMBE :
Juisi ya embe ikichanganywa na maziwa fresh husaidia kurejesha afya ya mtu aliye dhoofika.
Vile vile kunusa juisi ya embe kunasaidia kuzuia tatizo la kutoka damu puani. Hivyo basi juisi ya embe inaweza kutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu anaye tokwa na damu puani.
USHAURI
Unapotengeneza Juisi ya Maembe hakikisha huweki sukari kabisa, unapoweka sukari unapunguza nguvu ya Hii Juisi katika matibabu. Vilevile unapotumia Sehemu yoyote ya Mti huu au matunda hakikisha vipo katika hali nzuri usitumie vitu vilivyooza au kuharibika.
Dr Hamza
0654729438 WhatsApp coll sms
0655729439 coll sms
Tanga Pangani Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment