Zifahamu faida ya kutumia tangawizi katika mwili wa binadamu
Tangawizi ina faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo :
1. Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni,.
2. Kutibu tatizo la gesi tumboni
3. Kuondoa tatizo la msokoto wa tumbo (bila kuharisha)
4. Husaidia kuzuia kutapika.
5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli
6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
Jam ya tangawizi
Unaweza kutumia Jam ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali kama ilivyo onyeshwa hapo juu.
Jinsi ya kutengeneza Jam ya tangawizi
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
Muongozo wa kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia tangawizi
Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :
Kujitibu tatizo la kuvimbiwa na kukosa hamu ya kula
Changanya Juice ya Tangawizi, Juice ya Limau na Chumvi ya mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
Kujitibu tatizo la maumivu ya koo na kukauka sauti
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
Kujitibu tatizo la kuharisha
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.
Kichefuchefu na kuharisha
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.
Maumivu ya kichwa na wasiwasi
Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.
Maumivu makali ya tumbo
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
Baridi yabisi sugu
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.
Maumivu ya jino na kichwa
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.
==========
Tangawizi ni zao ambalo hustawi sehemu mbalimbali duniani na hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na pia kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali.
Zao hili lilianza kulimwa katika nchi za Asia, Afrika Magharibi na katika visiwa vya Caribbean. Tangawizi ni zao linalotumiwa na walaji wote ulimwenguni, hii inatokana na baadhi ya watu kutambua faida zake ki-lishe na kitiba.
Faida za tangawizi
Kitiba
Dozi ya tangawizi itolewe kulingana na uzito wa mtoto husika. Dozi nyingi za dawa za mitishamba hutolewa kwa kulinganishwa na dozi ya mtu mzima wa kilo 70, hivyo mtoto wa kilo 20 hadi 25 hupatiwa 1/3 ya dozi ya mtu mzima. Kwa ujumla kwa dozi ya mtu mzima huwa isizidi gramu 4 kila siku.
Ni vyema tukajenga mazoea ya kutumia dawa zitokanazo na mimea kama tangawizi kwa ajili ya kinga na tiba mbalimbali za miili yetu kwa sababu licha ya kuwa zinapatikana kirahisi pia si ghali na hazina madhara yeyote kwa afya zetu kama zilivyo dawa nyingi za viwandani.

- Katika lishe
Tangawizi ikichemshwa na maji na kuongezwa sukari hutoa kinywaji ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana. Baadhi ya watumiaji hupendelea kuongeza asali, vipande vya machungwa au limao ili kuweza kupata ladha nzuri zaidi. Vilevile hutumika katika utayarishwaji wa vinywaji vingine viwandani kama soda, chai, kahawa nakadhalika. - Hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali kama biskuti, mikate, keki, nyama na vingine vingi.
Kitiba
- Utomvu unaotokana na zao hili umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo vya binaadamu. Unapochua utomvu huu mara mbili kwa siku sehemu zenye maumivu huweza kuondosha maumivu mbalimbali haraka, kwa mfano maumivu ya misuli, magoti, maumivu ya kichwa nakadhalika.
- Hukinga na kutibu kuwashwa na kukereketwa koo (Sore throat) na ugonjwa wa mafua ya sehemu ya juu (Upper respiratory truck infection).
- Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.
- Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni. Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.
- Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.
- Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.
- Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo.
- Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.
- Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.
- Watu wengi ulimwenguni hutumia mmea huu kama dawa ya kuondoa harufu mbaya kinywani.
- Hutumika katika utengenezaji wa siki (vinegar) ambayo huhamasisha hamu ya kula
- Nchini China wanawake wengi wajawazito hutumia juisi ya tangawizi ili kujiepusha na adha ya kutapika mara kwa mara (Morning sickness).
- Tangawizi pia hutumika kama dawa ya kushusha joto la mwili na homa za mara kwa mara zinazosababishwa na malaria au mashambulizi ya bakteria na fangasi ambayo mara nyingi huchochea joto la mwili kupanda zaidi ya kiwango cha kawaida.
- Pia husaidia kushusha presha ya damu mwilini (hypertension) kwa watu wanaosumbuliwa na presha ya kupanda.
- Tangawizi pia hutumika kupunguza maumivu yanayosababishwa na matatizo ya mawe kwenye figo, vilevile hupunguza maumivu ya kibofu cha mkojo iwapo itatumika kuchuliwa kwa nje sehemu za mwili zilizo karibu na kiungo hiki.
- Virutubisho vilivyomo kwenye zao hili pia huhamasisha utendaji mzima wa vimengenyo mbalimbali katika usagaji wa chakula mwilini
na pia kutuongezea hamu ya kula chakula.
Dozi ya tangawizi itolewe kulingana na uzito wa mtoto husika. Dozi nyingi za dawa za mitishamba hutolewa kwa kulinganishwa na dozi ya mtu mzima wa kilo 70, hivyo mtoto wa kilo 20 hadi 25 hupatiwa 1/3 ya dozi ya mtu mzima. Kwa ujumla kwa dozi ya mtu mzima huwa isizidi gramu 4 kila siku.
Ni vyema tukajenga mazoea ya kutumia dawa zitokanazo na mimea kama tangawizi kwa ajili ya kinga na tiba mbalimbali za miili yetu kwa sababu licha ya kuwa zinapatikana kirahisi pia si ghali na hazina madhara yeyote kwa afya zetu kama zilivyo dawa nyingi za viwandani.
Dr Hamza
0654729438 WhatsApp SMS coll
0655729439 WhatsApp SMS coll
0746025804 coll SMS
Tanga Pangan Tanzania
0 comments:
Post a Comment