NYOTA YA MSHALE:
Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Novemba na 20 Disember
Asili yao ni Moto.Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 3
Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).
Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala alkhamisi aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor
Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea. Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Njano na Njano-machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva.
Kito (Jiwe) ni Feruzi (Turquoise) na Kito chekundu (Carbuncle).Madini yao ni Bati.
Manukato yao ni Yasmini (Jasmine), Manemane (Myrrh).
MAMBO MUHIMU:-
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa Kuongoza, Kuratibu, Kuandaa, Kupanga na Kusikiliza kwa makini.
Maadili yao ni Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kuwa na uwezo wa kusikiliza mawazo ya wenzake japokuwa siyo lazima akubaliane nayo.
Matakwa yao ni Kupanuka kimawazo.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutegemea mambo kuwa yatakuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha Ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.
USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba.
Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Samaki.
Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.
Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.
Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.
Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.
Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha.
Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Punda.
Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.
KIPAJI CHA MSHALE:
Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.(Prophetic)
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao.
Hawapendi mambo nusunusu.
Ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.
Mshale ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu,.hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake, mradi jambo hilo liwe la kweli.
Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe, huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.
Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali, inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
KAZI NA BIASHARA ZA MSHALE:
Mshale ni waaminifu wanaopenda sana mafanikio, wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.
Wenye nyota hii ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Wanawaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
MAVAZI NA MITINDO:
Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha kama koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi kama maua au nakshi nakshi.
Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti. Wanawake wapendelee kuvaa sketi.
MAGONJWA YA MSHALE:
Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.
Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.
Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysisi of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MSHALE:
Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mshale ni Bati. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Yakuti ya njano au Lapis Lazuli
MAFUSHO:
Mafusho ya Mshale ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
FUNGUO:
Funguo ya nyota ya mshale ni "nalenga" yeye akilenga kitu basi huwa hakosi hata akikipania
Dr Hamza
0654729438 coll,SMS WhatsApp
0746025804 coll,SMS
Tanga Pangan Tanzania
0 comments:
Post a Comment